
WATUMISHI wa tatu katika Halmashauri ya Sengerema Mkoani Mwanza wametunukiwa cheti cha heshima na Halmashauri kuu ya CCM wilaya humo kwa kusimamia vema miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao pamoja na kusimamia nidhamu.
Watumishi waliopewa vyeti hivyo ni Mkuu wa shule ya Katunguru Sekondari Baraka Msimba , Mkuu wa shule Sengerema Sekondari Zakaria Kahema pamoja na aliyekuwa meneja wa RUWASA Wilaya ya Sengerema Cassiani Wittike .
Akikabidhi vyeti hivyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema Marco Makoye amesema watumishi hawa kulingana na kazi walizofanya kwa weledi mkubwa kamati ya siasa ya wilaya ilipendekeza wapatiwa vyeti hivyo na Halmashauri kuu imethibitisha na kuwakabishi vyeti Ili iwe mfano kwa watumishi wengine.

Mkuu wa shule ya Sekondari Katunguru Baraka Msimba yeye amepewa cheti cha kusimamia nidhamu shule na kuongeza ufaulu sambamba na kujenga vyumba viwili vya madarasa kupitia mfumo wa P4R vilivyojengwa na kukamilika katika ubora.
Huku mkuu wa shule Sengerema Sekondari Zakaria Kahema yeye amepewa cheti cha usimamizi bora wa ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo imekamilika sambamba na kusimamia nidhamu ya walimu na Wanafunzi shule .
Aliyekuwa meneja wa RUWASA wilaya Sengerema, Cassian Wittike yeye amepewa cheti cha kusimamia na kukamisha miradi ya maji iliyokuwa imekwama kwa muda mrefu kwenye Halmashauri ya Sengerema pamoja na kukamilisha miradi ya maji Halmashauri ya Buchosa ambapo maji yanapatika kwa asimilia 54 hadi Sasa.

Kwa upande wa wanasiasa waliopewa vyeti hivyo ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Yanga Makaga ambaye amepewa cheti cha kujitoa kukisaidia chama Cha Mapinduzi zaidi ya sh. milioni 10, zilizotumika kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya CCM wilayani humo sambamba na mwenyekiti wa CCM wilayani humo Marco Makoye ambaye amepewa cheti cha uongozi bora na kuhakisha ofisi ya CCM inakamilika na wanahamia.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Sengerema George Kazungu amesema watumishi hawa walipaswa kupata vyeti hivyo na isiishie hapo.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wa wenzake mkuu wa shule ya Sekondari Katunguru Baraka Msimba amesema nidhamu ya kusimamizi wa fedha ubunifu na kukamilisha miradi ya maendeleo kwa weledi ndiyo siri ya mafanikio ya wao kufika hapa walipofika leo.
“Hatutarudi nyuma katika suala zima la kusimamia Mali za umma Ili ziwanufaishe Wananchi”alisema Msimba.
Katika hatua nyingine mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Sengerema ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga amesema chama cha Mapinduzi nimefanya Jambo jema la kuwatunuku vyeti watumishi hawa kulingana kazi zao wanazofanya zinazoonekana machoni kwa watu .