
Gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T872CHR limetumbukia baharini jana saa saba katika eneo la Ufukwe wa Coco, jijini Dar Es Salaam.
Mashuhuda wanasema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na kwamba gari hilo lilimshinda uthibiti dereva ambaye jina lake halikufahamika huku taarifa zikisema aliokolewa akiwa mahututi.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Uokoaji na Utunzaji Mazingira eneo la Coco, Ahmed Abdallah alisema alipigiwa simu na vijana wake kufahamishwa juu ya ajali hiyo ambapo alifika na kuungana nao katika uokoaji uliochukua zaidi ya saa nne.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Oktoba 5,2021 na kwamba hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya dereva wa gari hilo kuokolewa.

Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.
“Kule alipokuwa anakwenda kulikuwa hakuna barabara, kama mtu ni mzima huwezi kuona gari linakwenda baharini na wewe ukazidi kukanyaga mafuta”,amesema Kingai.
@manyota_rich
View this post on Instagram