
WAKATI Kampeni za uchaguzi nchini Ufilipino zikikaribia kufika tamati na mgeni ambaye alikuwa hajaalikwa aliamua kumtembelea rais wa nchi hiyo pasi na kualikwa.
Rais Rodrigo Duterte alikuwa katika harakati za kukamilisha hotuba yake iliyochukua saa nne ambapo alikuwa anawapigia debe wagombea wa chama tawala mnamo Jumatano, Mei 8, 2019 wakati alipopigwa na duwaa baada ya kuona mende akipeperuka kutoka kwenye nguo yake.
Huenda mdudu huyo alivutiwa na mwangaza wa picha zilizokuwa zinapigwa na papo hapo akajitokeza ghafla ndani ya nguo aliyokuwa ameivaa Rodrigo na kuanza kumtambalia huku akizua sintofahamu miongoni mwa kikosi cha rais huyo.
Mdudu huyo alitambaa kifuani kwa Rais Duterte kwa ujasiri na hata juhudi za mmoja wa walinzi wake wa kike za kumuondoa ziligonga mwamba.
Mende huyo aliyekuwa mkubwa alizidi kumtambalia rais na kutatiza hotuba yake wakati akijaribu kumuondoa. Mwanasiasa huyo wa miaka 74, aliwatania wapinzani wake na kudai kuwa mende huyo alitoka mrengo wao.
Dondosha comment yako hapa