
RAPA maarufu duniani kutoka nchini Marekani, Cardi B amewafurahisha Wakenya kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutupia video ya mwaka 2009 ya rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki alipokuwa akitangaza kuwa ana mke mmoja tu.
Rais Kibaki aliamua kuanika hayo tena mbele ya mke wake baada ya kuchoshwa na tuhuma za waja kwamba alikuwa na mke wa pili.
Mke wake, Lucy Kibaki, alikuwa amesimama kando ya mume wake alipokanusha taarifa za kuwa na mke wa pili. Alivitaka vyombo vya habari kutaka ufafanuzi akisema vilikuwa vikieneza uongo.
Haijafahamika kwa nini Card B aliamua kutuma video hiyo ya maktaba kupitia akauntiu yake ya Twitter jana Jumatatu.
Ujumbe huo ulikuwa na maelfu ya kauli za Wakenya kwenye Twitter, waliokuwa wakiwasaidia wale ambao hawakuelewa dhana ya video hiyo na wengine waliongezea kauli zao. “Siku nzuri za zamani… uchumi ulikuwa juu ila tu maigizo yalikuwa katika nyumba kubwa…’’ mtangazaji wa redio wa Kenya radio Shaffie Weru aliandika katika ujumbe wake wa Twitter.
— iamcardib (@iamcardib) October 4, 2021