×

Hukumu Kesi Ya Aveva, Kaburu Ngoma Nzito..

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake kutokana na Mshtakiwa Aveva kutokuwepo kutokana na kwenda katika Matibu Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya washitakiwa kumaliza kujitetea.

 

Mbali na Aveva washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange (Kaburu) ambaye alikuwa Makamu pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Pope, ambaye  hivi sasa ni marehemu.

 

Kabla ya kuanza kusikilizwa hukumu hiyo Hakimu alimuuliza Mshtakiwa, Nyange juu ya mshtakiwa mwenzake alipo ndipo akasimama na kuiambia mahakama kuwa amehudhuria Hospitali ya Taifa Muhimbili kuendelea na matibabu ambayo alipangiwa kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Baada ya kueleza hayo hakimu Simba akaiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21,2021.

 

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulikuwa na jumla ya mashahidi 10 na vielelezo mbalimbali huku washitakiwa wakijitetea wenyewe.

 

Mashtaka hayo ni pamoja na yakula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutoa maelezo ya uongo.

Katika shitaka la kughushi ilinawakabili  washitakiwa wote, wanadaiwa walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

Leave a Comment