×

Mtibwa Waziita Yanga, Simba Manungu

MTIBWA Sugar imesema kwamba, ipo kwenye hatua nzuri ya kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Manungu ili waweze kuutumia kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya timu zote ikiwemo Simba na Yanga.

Uwanja huo wa nyumbani wa Mtibwa, ulifungiwa msimu uliopita na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na kutokidhi vigezo na kuifanya timu hiyo kubadilisha uwanja kwa kuutumia Jamhuri.

Msimu huu, Mtibwa imeshindwa pia kuutumia Uwanja wa Jamhuri, ambapo katika mechi zake mbili za kwanza za Ligi Kuu Bara, imetumia Uwanja wa Mabatini uliopo Pwani na Uhuru, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Kuhusu uwanja wetu wa Manungu uliopo Turiani, tumeshakamilisha marekebisho ya eneo la kuchezea na tayari tumeweka uzio.

“Kinachoendelea kwa sasa ni ujenzi wa ukuta ambao utachukua wiki nne kukamilika, hivyo tunatarajia mechi za Simba na Yanga tutacheza kwenye uwanja wetu.”

LEEN ESSAU

Leave a Comment