×

Ni Mayele Tena

TIMU ya soka ya Mbeya City kupitia kwa kocha wake msaidizi Mathias Wandiba, amesema timu yake inaendelea na maandalizi makali jijini hapa lengo ikiwa ni kuhakikisha inapata matokeo mbele ya Kagera Sugar kwenye Ligi Kuu Bara.

Wandiba ameliambia Championi kuwa :“ Ni kweli kwa sasa tuko Mwanza tukijiandaa na mchezo wetu na Kagera Sugar kimsingi utakuwa mchezo mgumu ambao tunapaswa kushinda ili kutafuta pointi mapema hivyo naamini tutashinda mbele ya Kagera Sugar”

“Tutakua na takribani siku nne za kukaa Mwanza huku tukifanya mazoezi makali na kwakuwa mchezo wetu umepangwa kuchezwa saa 8 mchana na mazoezi yetu yataendana na wakati huo.”

Leave a Comment