Global Tv imefunga safari mpaka Kimara Michongwani na kukutana na familia ya Mzee Simoni na Mama yake wote wagonjwa, Global Tv tukafanya mazungumzo na familia hii ambapo Mzee SAIMON amepatwa na tatizo la uvimbe mwilini mwake chanzo akieleza ni kijipu kidogo kilichomtokea, yupo kitandani mwaka sasa hajiwezi, hatembei pia mama yake mzazi mgonjwa nae hawana msaada na hali zao sio nzuri.