
MSANII Adele Laurie Blue Adkins amerejea kwa kishindo baada ya miaka sita ya ukimya na kudondosha ngoma mpya “Easy On Me” wimbo nyororo inayosindikizwa na kinanda, ambayo ameiachia jana huko Uingereza.
Ikiwa ni inatoka kwa mara ya kwanza ndani ya miaka sita ya ukimya, mashabiki walipata albumu ya “Divorce” inaingia kwenye orodha ya albamu zake zenye mafanikio makubwa kulingana na mapokezi yake.
“Easy On Me” inayoelezea kwa namna ambavyo maisha yake ya sasa yanavyosonga baada ya kuondoka kwenye ndoa yake mwaka 2019.
“Nilibadilisha maamuzi kila mara, “lakini sasa nimeamua tuachane,” sehemu ya mashairi ya wimbo huo anaimba Adele. Katika video ya muziki, muongozaji mkuu Xavier Dolan alichagua kuwepo kwa rangi mbili ili ziendane na uhalisia ambazo ni rangi nyeusi na nyeupe.
Adele anaingia kwenye historia nyingine ya kuwa mwanamuziki mwanamke aliyeweza kurudisha ladha ya mziki wake baada ya muda mrefu.
Adele ameelezea zaidi juu yake na familia yake kupitia kwenye nyimbo yake huku akidhani kuwa ni muda sahihi kwake kufikiri hivi.
“Nilikuwa na nia njema, matumaini makubwa, lakini kwasasa yamepotea kabisa.” Wimbo huo ni wa kwanza kuandikwa katika albamu inayokuja ya Adele, na alianza kuuandika mwaka ambao aliachana na mume wake.