
ALIPOAMBIWA ajitete; aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu yuko kwenye mipango ya kuoa na kwamba tayari ameshamtolea mahari mchumba wake.
Hata hivyo, mahakama ilimhukumu kifungu cha miaka 30 jela kwa kumkuta na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hebu jivike Usabaya, uangalie namna ndoto za maisha yako zilivyozimika ukiwa na umri mdogo, iangalie familia aliyoiacha nyuma yake. Baada ya hapo jiweke upande wa Washtaki kwamba waliporwa mali zao kwa nguvu wakadhalilishwa na kuonewa kwa mtutu wa bunduki.
Shusha hapa nchini komenti zako zitaonekana ulimwenguni kote.
@manyota_rich