
Innocent Matara-Global TV- Nairobi, Kenya Mwaka 2010 nchini Kenya iliwahi kuripotiwa stori ya wanawake zaidi ya kumi kuuawa na baadaye muuaji alijitangaza na kukiri kuwa yeye ndiye muuaji wa hao wanawake.
Matukio hayo yaliripotiwa katika jiji la Nairobi Kenya na katika maeneo ya Rift Valley. Tukio kama hilo limetokea tena Ruiru, Kaunti ya Kiambu ambapo jeshi la polisi linamshikiria mwanaume mmoja aliyetambulika kama Paul Magara, 29 kwa tuhuma za kuwachoma visu, kuwabaka na kuwaua wanawake katika kijiji cha Wataalam. Baaada ya polisi kupata taarifa za kiintelejensia walianza upeleleizi wao na kufanikiwa kumdaka bwana Magara, na jambo la ajabu ni begi alilokutwa nalo likiwa na nguo za ndani za wanawake, alizodai kuzitumia kujifutia jasho.
Huyu hapa Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Ruiru Cecilia Kemboi anafafanua kuhusu tukio hilo.