Rais Samia Azindua Hospitali Ya Jiji La Arusha – (Picha +Video)
Global Publishers October 17, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Rais Samia akikata utepe kuzindua rasmi Hospitali ya Jiji la Arusha katika Eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Oktoba, 2021 amezindua rasmi Hospitali ya Jiji la Arusha katika Eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha.
Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.
Rais Samia, akimsalimia mtoto Samia Yona aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi Mary Joseph (34) mkazi wa Njiro Arusha. Rais Samia, akimsalimia mtoto Nassir Mbarouk aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha leo tarehe 17 Oktoba, 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi Shadya Samson (32) mkazi wa Uswahilini Arusha.Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi Mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa TAMISEMI Ummy Ally Mwalimu alipowasili Kufanya Uzinduzi wa Hospitali ya Jiji la Arusha Eneo la Njiro Mkoani Arusha