
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amehutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo tarehe 17 Oktoba, 2021 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.



