×

Rais Kenyatta Aondoa Masharti ya Kutotoka Nje

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameondoa masharti ya kutotoka nje usiku kwa wananchi wake ambayo yaliwekwa  tangu Machi 2020 ili kupambana na corona.

 

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha siku kuu ya mashujaa, Uhuru amesema kwamba hatua hiyo inafuatia kupungua kwa visa vya maambukizi ya covid-19 nchini Kenya.

 

Amesema kwamba kufikia sasa ni watu milioni 5 waliopata chanjo ya ugonjwa wa corona. Kenya inapania kuwapatia chanjo watu milioni 10 kufikia Disemba mwaka huu.

 

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo Wakenya wamekuwa wakiitaka serikali kuondoa masharti hayo kwa lengo la kuendelea na biashara zao za kawaida.

Leave a Comment