Sensa ya mwaka 2022, itafanyika kidigital. Hayo yamesemwa na aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda katika uzinduzi wa mafunzo ya washiriki wa utafiti wa majaribio wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria Tanzania wa mwaka 2021-22 ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro.