×

Wanawake Tulikuwa Kama Daraja, Leo Tuko Wenyewe – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) iliyoambatana na kumbukizi ya Kumuezi Bibi Titi Mohammed Mwenyekiti wa kwanza wa UWT. Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 23 Oktoba, 2021 katika Uwanja wa Ujamaa Umwe Kusini Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kwa muda mrefu wanawake wamekuwa kama daraja la kuvusha vongozi wengine huku wanawake wakibaki nyuma lakini sasa ni wakati wawanawake kushika nyadhifa za juu na kuonyesha uwezo wao wa kiuongozi.

 

Raios Samia amesema hayo leo Jumamosi, Oktoba 23, 2021 wakatio akituhubia katika Kilele cha Wiki ya Umoja wa Wanawake (UWT) na kumuenzi Mwenyekiti wa Kwanza wa Umoja huo ambaye pia alikuwa mwanaharakati  wa kupigani ukombozi, marehemu Bibi Titi Mohammed.

 

“Tumekutana hapa kwa madhumuni makuu mawili, moja ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya UWT Kitaifa na jambo la pili ni kumuenzi Hayati Bibi Titi Mohamed na tena aenziwe hapa nyumbani kwake Rufiji. 

 

“Bibi Titi Mohamed alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wanawake na wanaume katika harakati za kupigania uhuru na kujiunga na TANU, kwa kutembea kwa miguu kwenda kuwahimiza. Hatuwezi kuzungumzia harakati za Mwalimu Julius Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika bila kutaja jina la Bibi Titi Mohamed.

 

“Alipokuwa mbunge, Bibi Titi alipigania maslahi ya wanawake na kudai fursa sawa katika masuala ya elimu, ajira na uongozi. Kipindi hicho cha Bibi Titi Mohamed akipigania haki za wanawake hata mataifa mengine ya Ulaya yalikuwa bado hayajaanza harakati hizi.

 

“Historia ya Bibi Titi Mohamed imeandikwa katika kurasa chache sidhani kama imetosha. Nitoe rai kwa watafiti na waandishi wa masuala ya siasa na jamii wafanye hivyo ili jamii iweze kuujua mchango wa marehemu Bibi Titi Mohamed kwa jamii na Taifa.

 

“Tumekusanyika hapa si tu kumsifu ili tumsifu, bali tumsifu kwa lengo la kwenda kujipaga kwa matendo yetu yaendane na dhamira ya shujaa wetu huyu Marehemu Bibi Titi. Taasisi ya UWT chini ya Chama Cha Mapinduzi iliundwa kwa lengo la kumkomboa mwanamke kisiasa, kijamii na kiuchumi pamoja na kuwaunganisha wanawake wa Tanzania.

 

“UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi wa serikali pamoja na Jumuiya yetu. UWT tangu kipindi kile ikiitwa tawi la TANU imeweza kubadilia mitazamo ya wanawake na kutoka kule ilipokuwa na kupiga hatua ya kuweza kuendesha mambo yao wenyewe.

 

“Kwa miaka mingi, wanawake tulikuwa kama daraja la kutengeneza viongozi wa Taifa hili na kwa kudra ya Mungu leo tuko wenyewe, ndugu zangu tushirikiane na tuwe wa moja ili kutimiza matarajio ya Jumuiya yetu pamoja na matarajio ya Taifa letu.

 

“UWT inapata changamoto nyingi ikiwemo ukatili wa kijinsia, nadhani sisi nao tujachangia. Kama tungelipinga hilo lisingelitokea, haipendezi kuona mwanamke mwenzako akifanyiwa vitendo hivyo vya ukatili, kwa kuwa haujafanyiwa wewe.

 

“Umoja wa Wanawake Tanzania chini ya Chama Cha Mapinduzi tuendelee kuwa imara na tujisahihishe pale tunapokosea ili twende na safari ya kumkomboa mwanamke kisiasa, kijamii, kifikra na kiuchumi.

 

“Tukisimama pamoja tutaondoa hiliBilioni 13.39 zitatumika Mkoa wa Pwani kujenga vyumba 429 vya madarasa kwa shule za sekondari, na madarasa 108 katika vituo shikizi vya shule za msingi, na fedha hizi ni zile za kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19Ukiondoa Mkoa wa Dar es Salaam.

 

“Mkoa wa Pwani ni katika mikoa iliyopata mgao mkubwa wa fedha za kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19, umepata kasi cha Tsh bilioni 13.39.

“Kutokana na hali tuliyokuwa nayo hatuwezi kugawa maeneo mapya mengine kwa ajili ya utawala.Kutokana na hali tuliyokuwa nayo hatuwezi kugawa maeneo mapya mengine kwa ajili ya utawala. 

 

“Niwakumbushe kuendeleza kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 na kufuata ushauri wa wataalam wetu. Tutakapochanja tutakuwa na kiwango kikubwa cha usalama, si kwamba ukishachanjwa hautapata lakini pia hata ukipata hautakuletea madhara makubwa,” amesema Rais Samia.

Leave a Comment