
Rapa wa Kimarekani, Young Thug ameishtaki kampuni ya makazi inayomiliki ghorofa la Concierge ambapo alikuwa anaishi, kwa kumruhusu mtu asiyefahamika kuingia ndani na kutoka na begi la rapa huyo ambalo lilikuwa na nyimbo 200 ambazo bado hakuziachia, vito vya thamani kama almasi pamoja na pesa ambazo kwa pamoja zina thamani ya zaidi ya dola 100000 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya milioni 200 za Kitanzania.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyofikishwa mahakamani, yanaonesha kuwa Nov 1, 2020 Young Thug alihifandhi begi lake sehemu salama lakini baadaye alipotoka nje alikuta tayari mfanyakazi wa ghorofa hilo ameshamkabizi mtu mwingine tofauti.
Begi hilo lililopotea lilikuwa na flash yenye nyimbo 200 ambazo zilikuwa mbioni kuachiwa na msanii huyo, ambazo zinathamani ya dola milioni 1 za kimarekani zaidi ya bilioni 2 za Kitanzania, pia begi hilo lilikuwa na pesa na madini ya almasi ambayo kwa pamoja yanathamani ya zaidi ya milioni 200 za Kitanzania.
Cc; @bakarimahundu