×

Tunda: Ni Rasmi Sasa Nipo Singo

MUUZA sura (video vixen) maarufu kwenye video za muziki za wasanii wa Bongo Fleva, Annastazia Kimaro ‘Tunda’ ameweka wazi kuwa, ni rasmi yupo singo hivyo wanaume wasijichanganye kwake.

 

Kauli hiyo tata aliitoa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat na kuacha watu midomo wazi kwani wengi wao wanajua kuwa bado yupo kwenye mahaba mazito na baby daddy wake, Whozu ambaye amezaa naye mtoto mmoja aitwaye Lolla.

 

“Ukiniona ni kama kweli nina boyfriend mpya kumbe ni drama tu nafanya, nipo singo msijichanganye,” anasema Tunda.

 

GLOBAL PUBLISHERS ilimtafuta Tunda kutaka kujua ukweli wa jambo hilo, lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

 

Kumekuwa na tetesi za wiki kadhaa kwamba, huwenda Tunda ameachana na Whozu kutokana na namna mrembo huyo anavyojichanganya na wanaume wengine, tofauti na alivyokuwa bize na jamaa huyo.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment