
IKIWA ni muendelezo wa kesi namba 16/2021 ya Uhujumu Uchumi na makosa ya kupanga njama za kupanga kutekeleza matukio ugaidi na kufadhiri ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu hatimaye shahid wa 7 upande wa Jamhuri amewasili mahakamani leo Novemba 5, 2021 kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.
Shahidi wa saba aliyejitambulisha kama Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Omary Mahita ambaye anafanya kazi Idara ya Upelelezi, mwenye umri wa miaka 36 akiongozwa na Wakili wa Serikali, Pius Hilla ameieleza mahakama namna alivyohusika katika tukio la ukamataji wa watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa katika kesi hiyo.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Joachim Tiganga, Inspekta Mahita amesema alipewa maelekezo ya kuunda kikosi maalum ili kukitia nguvuni kikundi cha watu (watuhumiwa ambao ni Mbowe na wenzake, Halfan Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo ) ambacho amedai kilikuwa kinataka kufanya vitendo vya kigaidi maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya.
Ametaja vitendo hivyo vya kihalifu ni kuchoma vituo vya mafuta, kuzuia barabara, kukata miti, kufanya maandamano yasiyo na kikomo pamoja na kumdhuru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya hai kwa Kipindi hicho Lengai Ole Sabaya. Mpaka sasa, Inspekta Mahita bado yuko kizimbani anaendelea kutoa ushahidi wake.
SEHEMU YA USHAIDI HUO
Jaji: Majina yako
Shahidi: Inspector Mahita Mohamed
Jaji: Umri
Shahidi: 36
Jaji: Kabila
Shahidi: Mluguru
Jaji: Kazi
Shahidi: Askari Polisi
Jaji: Dini
Shahidi: muislam
Shahidi: Wallah wabillah watallah, Nathibitisha Kutoa Ushahidi Wa Kweli
Wakili wa Serikali: Ataongozwa na Wakili Pius Hilla
Wakili wa Serikali: Mahita Wewe ni Mkazi wa wapi
Shahidi: Mkazi wa Morogoro
Wakili wa Serikali: Tangu lini
Shahidi: Mwezi 04 Mwaka 2021
Wakili wa Serikali: Kabla Mwezi wa Nne ulikuwa Ukiishi wapi
Shahidi: Arusha
Wakili wa Serikali: Kazi yako ni Ipi
Shahidi: Polisi
Wakili wa Serikali: Tangu lini
Shahidi: Mwezi wa 03 2011
Wakili wa Serikali: Upo Kitengo gani
Shahidi: Idara ya Polisi Upelelezi wa Jinai
WS: Kwa Muda gani
Shahidi: Kwa Miaka 08
WS: Arusha Ulikwenda Lini
Shahidi: Tangu Mwaka 2014
WS: Mwaka 2020 ulikuwa kituo gani
Shahidi: Central Police Arusha
WS: Ulikuwa na nafasi gani
Shahidi: Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha
WS: Ieleze Mahakama ukiwa Kama Afisa wa Polisi Majukumu Yako yalikuwa ni yapi
Shahidi: Ukamataji wa wahalifu, Upekuzi wa tuhumiwa na Maeneo, Kusafirisha Watuhumiwa
WS: Unamaanisha Nini
Shahidi: Kuwatoa Watuhumiwa kuwatoa na kuwapeleka Sehemu Nyingine
WS: Kingine
Shahidi: Kuzuia na Kupambama na Uhalifu
WS: Kingine
Shahidi: Uandishi Wa Maelezo, ya Mashahidi na Watuhumiwa pamoja na Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Kusimamia Askari waliopo Chini yangu
WS: Tarehe 04 August 2020 nini Kilotokea
Shahidi: Nikiwa Ofisini Arusha Nilipogiwa Simu na Afande Wangu ACP Ramadhan Kingai, aliniita Ofisini kwake
Aliniagiza Kutafuta Askari Wawili
Ambapo niliwatafuta Detective Francis na koplo Goodluck
Tulienda Ofisi ya Afande RCO akatuambia tunatoka Kwa ajili ya Safari ya kazi
Kuna kazi ya kwenda Kufanya
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi
Shahidi: Saa 11
Wakili wa Serikali: Kingai alisema mnapenda Kufanya kazi wapi
Shahidi: Tunaenda Kufanya kazi Moshi
WS: Ukiwa pale sasa na Goodluck pamoja na Francis kitu gani kilifuata
Shahidi: Tulijiandaa na Safari pamoja na Askari Mwingine anayetokea Ofisini Kwake
ASP Jumanne alikuwa na Yeye anatusubiria pale tujiunge naye kwa Pamoja twende Moshi
Alikuwa anatusubiria Arumeru
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Arumeru Mlielekea Wapi
Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya
Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya
WS: Nani aliye fanya Briefing Siku hiyo
Shahidi: Afande Kingai ambaye ndiye alikuwa Kiongozi wetu wa Msafara
Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani
Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo
MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz
Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi
WS: Vitendo gani hivyo
Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya
Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi
Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya
Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo
WS: Aliwataja akina nani
Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Kwa taariza zaid ya kinacheondelea kujiri mahakamani katika kesi ya Freeman Mbowe, Dar es Salaam na ileya Lengai Ole Sabaya kule Arusha, tufuatilie katika tovuti yetu na Instagram page yetu ya GlobalPublishers.