×

Petitman: Nipo na Maskini Mwenzangu

MENEJA wa wasanii mbalimbali Bongo, Hamad Manungwi almaarufu Petitman amefunguka kuwa, kwa sasa hana msongo wowote, wala kufikiria chochote kutoka kwa mzazi mwenzake wa hivi sasa aitwaye Dodo kwa sababu wote ni maskini na wanameridhika na hali zao na Mungu alivyowajalia zawadi ya mtoto ikawa baraka zaidi kwenye ndoa yao.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Petitman ambaye ni zaidi ya mwaka na nusu tangu alipotengana na mama wa mtotp wake wa kwanza, Esma Platnumz ambaye ni dada wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, anasema kuwa, hakuna kipindi anachoishi kwa furaha kama anavyoishi hivi sasa kwani kinachopatikana anafurahi pamoja na familia yake na si kitu kingine.

 

“Mungu ni mkubwa sana sijui nisemaje, lakini ukweli nafurahia sana maisha yangu ya sasa, nipo na maskini mwenzangu, mke wangu mtatarajiwa pamoja na mtoto wetu kwani kinachopatikana hakika tunafurahi na tunakubaliana na hali zetu na wala hatuhitaji vitu vya juu maana maisha yetu ya kimaskini yanatutosha,” anasema Petitman ambaye wakati akiwa na Esma aliambia yupo naye kwa sababu ya pesa za mwanamama huyo ambazo zinatokana na Diamond.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment