×

Wanne Wafariki, 300 Wajeruhiwa Tamasha la Travis Scott

WATU wanane wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati waufunguzi wa Tamasha la muziki la msanii Travis Scott lililoitwa Astroworld huko Houston, Texas nchini Marekani jana Ijumaa, majira ya saa 3:15 usiku.

Imeelezwa kuwa maafa hayo yametokana na kundi la watu waliohudhuria tamasha hilo lililokuwa na watu zaidi ya 50,000 kuanza kusongamana kuelekea mbele ya jukwaa, kubanana na kuanza kukanyagana. Imeelezwa kwamba, watu 11 wamelazwa hospitali kutokana na mshtuko wa moyo, watu 300 wamepata majeraha mbalimbali.

 

Travis Scott alilazimika kusitisha Tamasha hilo baada ya kushuhudia mashabiki wake wakiwa kwenye taharuki na wengine wakiwa wamejeruhiwa. Astroworld ni Tamasha la kila mwaka inayofanyika katika bustani ya NRG tangu mwaka 2018, ingawa ilisitishwa mwaka jana kwa sababu ya janga la Covid-19.

Leave a Comment