
MSANII wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya ECB, Raymond Mwakyusa ndiye msanii wa pili kwa idadi kubwa ya watazamaji wa jumla (total views) katika Mtandao wa YouTube Afrika Mashariki akiwapoteza kabisa wenzake wakubwa kama Rajab Abdul au Harmonize na King Kiba.
Rayvanny au Vanny Boy aliyejiunga na mtandao huo Machi 17, 2016 anachukua nafasi hiyo ya pili akiwa na jumla ya views zaidi ya million 643.8 baada ya kumpita Harmonize au Harmo ambaye alijiunga mwaka mmoja nyuma yake na sasa ana jumla ya views milioni 643.7.
Mpaka sasa, Diamond Platnumz ndiye kinara wa jumla wa views kwa nchi zinazopatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika akiwa na jumla ya watazamaji zaidi ya bilioni 1.5.
STORI; KHADIJA BAKARI, DAR