
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limemdaka mzee (70) anayejulikana kwa jina la Sanani Seif Juma mkazi wa Chamboni, Wilaya ya Micheweni kwa tuhuma ya kumlawiti mtoto wa miaka 14, ambapo mwenyewe alipohojiwa alikiri kufanya unyama huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis amesema, tukio hilo limetokea Novemba 6 mwaka huu, huku akidai kuwa maelezo ya mtuhumiwa yameonesha kuwa amekuwa akimfanyia mtoto huyo kitendo hicho mara kwa mara.
Daktari kutoka Hospitali ya Wilaya ya Micheweni, Zuberi Omar Zubeir amesema vipimo vinaonesha kuwa tayari mtoto huyo ameharibiwa jambo ambalo limemkasirisha Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Mgeni Khatib Yahya ambaye amevitaka vyombo vya usalama kumbana zaidi mtuhumiwa ili kubaini kama kuna watoto wengine amekuwa akiwafanyia mchezo huo wa ovyo.
Dunia inaelekea wapi; hebu weka komenti zako hapa chini ukishauri nini kifanyike kukomesha vitendo hivi vibaya hasa kwa watoto?
@manyota_rich #globalpublishersupdates