×

Mwalimu Mbaroni kwa Kumuoa Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza


MWALIMU wa Shule ya Msingi Itete, Kata ya Kirando wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuoa na kumuweka unyumba mwanafunzi aliyehitimu darasa la saba Jeska Mwanji (20),  ambaye anatarajiwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwakani, 

 

Mwalimu Mwanakurya anadaiwa kumuoa mwanafunzi huyo tangu mwaka jana 2020 na kuishi nae katika nyumba za Serikali zilizopo Katika Shule ya Msingi Itete aliposomea mwanafunzi huyo kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza.

Mbali na mwalimu Mwanakurya, pia mwalimu mkuu wa shule hiyo naye alikamatwa kwa ajili ya kuhojiwa na baadaye aliachiwa huru.

 

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ametoa rai kwa wanachi kupeuka tamaa ya kupokea Mali na kuamua kuwaozesha watoto wao na kukatisha ndoto zao.

 

Lijualikali ameongeza kuwa, walimu wa Shule za msingi na sekondari waziheshimu sketi za shule kwani zitawaletea matatizo katika kazi zao.

 

Novemba 1, 2021, DC Lijualikali alianza oparesheni maalum ya kuzuia na kupambana na mimba za utotoni ambapo oparesheni hiyo endelevu itawabaini walioachiswa shule na kuolewa.

Leave a Comment