
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene ameendelea kusisitiza wananchi wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kabla muda uliotolewa kisheria kumalizika.
Amebainisha hayo jijini Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ambayo imehusisha ukagua wa ghala la silaha za polisi ambalo limehifadhi pia silaha zaidi ya hamsini zilizosalimishwa na wakazi wa mkoa wa Arusha.
Simbachawene amesema mkoa wa Arusha umeongoza katika zoezi hilo ambapo amewataka Viongozi wa Serikali ikiwemo wakuu wa mikoa na Wilaya kuungana na jeshi la polisi katika kampeni ya kuwahamasisha wananchi wanaomiliki silaha isivyo kihalali kuzisalimisha.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha amesema mwitikio waliouonesha wananchi unatokana na kampeni za uhamasishaji ambazo wanaendelea kuzifanya kila Mara tangu msamaha huo utolewe.