
Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Hamis Juma kufuatia kifo cha jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Njengafibili Mponjoli Mwaikugile kilichotokea leo Novemba 20, 2021 jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha jaji huyo kwa majonzi na masikitiko makubwa kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa.
Amewapa pole wanafamilia wote na kuwaomba wae na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kumuombea marehemu apumzike mahali pema peponi.