
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Real Madrid, Karim Benzema amepatikana na hatia ya kula njama za kuvujisha video ya ngono ya mwanasoka mwenzake wa Ufaransa.
Benzema, mwenye umri wa miaka 32, anadaiwa kuvujisha picha za video za Mathieu Valbuena, bila kumuhusisha muhusika hali ambayo ilipelekea jeshi la polisi kuingilia kati kutokana na mashitaka yaliyofikishwa mezani kwao.
Hata hivyo imeelezwa kwamba wawili hao ni marafiki wa karibu, na hatua hiyo ilichagiza picha hizo kumfikia kwa urahisi Benzema.
Jaji alimpa Benzema kifungo cha mwaka mmoja jela na kuamuru alipe faini ya €75,000 (Tsh milioni 193). Benzema alikuwa mmoja wa watu watano walioshtakiwa kwa jaribio la kutoa fedha ili kutaka kuzima sakata hilo.
Kashfa hiyo imeshangaza jamii ya soka nchini Ufaransa na wachezaji wote wawili kupoteza nafasi katika timu yao ya taifa. Kesi hiyo ilianza Juni 2015, wakati wanasoka hao wawili walikuwa kwenye kambi ya mazoezi ya Ufaransa.
Katika kambi hiyo, Benzema aliweka shinikizo kwa Valbuena kuwalipa watu waliodai kuwa na kanda hiyo, ambao alikuwa amefanya nao njama ya kuwa mpatanishi, waendesha mashtaka walisema.
Benzema amekuwa akikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa alikuwa akijaribu tu kumsaidia Valbuena kujiondoa kutoka kashfa ya video hiyo iliyomtia hatarini