
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Tulia Ackson,ambaye pia Mbunge wa Mbeya Mjini, leo Disemba 24,amezindua maadhimisho ya siku ya UKIMWI Dunia,ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Disemba 1,katika viwanja vya Luandanzovwe,Mkoani Mbeya, ambapo katika uzinduzi huo ulioudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serekali na kukafuatiwa na harambe kwaajili ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI wa ATF, ambayo iko chini ya Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) baadhi ya makampuni mbalimbali kama Star Times,imechangilia milioni Hamsini, GGM,imechangia pia milioni Hamsini,na Tulia Trust,ilichangia milioni tano na baadhi ya watu wengine walitoa viwango tofauti tofauti.

Tulia pia alisisitiza wanaume kufanya tohara ambao bado hawajafanya hivyo,ili kuepuka magonjwa ya maambukizi ikiwemo VVU,na huduma hiyo ilikuwa ikitolewa kwenye viwanja hivyo,na kuongeza kuwa wananchi wa Mbeya,wakae tayari kumpokea Rais wetu Samia Suluhu Hassan,ambaye anatarajiwa kuwa ndio mgeni rasmi siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya UKIMWI, ambapo kauli mbiu ni Zingatia usawa,Tokomeza UKIMWI,Tokomeza magonjwa ya mlipuko.