
MWANAMITINDO wa kimataifa wa Bongo, Fahyma amethibitisha kwamba hapoi wala haboi baada ya kudai yeye bado ni mrembo mbichi.
Fahyma ambaye ni baby mama wa Rayvanny ameendelea kutupia picha mpya kwenye Instagram yake zinazomuonesha akizidi kung’ara na kuwa mtamu zaidi kuanzia umbo, sura ya kitoto na kuzidi kupendeza zaidi ambapo baadhi ya mashabiki wake wake wamekuwa wakimsifia nay eye mwenyewe kuwajibu; “Mimi Bado mtoto mbichi…”
Mwanamama huyo amekuwa midomoni mwa wengi baada ya kuachwa na Rayvanny ambaye sasa anajivinjari na mtoto Paula Kajala aliyeko masomoni nchini Uturuki.