×

Mama Azaa Watoto 3 Wote Walemavu Wa Akili, Yeye Akatwa Mguu-Video

Familia ya Bi Asha Hamis Juma na mumewe Ally Mohamed Ally, wakazi wa Konde, Micheweni kisiwani Pemba, wanaishi katika dhiki kubwa kufuatia watoto wao watatu, kusumbuliwa na ulemavu na ugonjwa wa akili uliowapata tangu walipozaliwa.

Hali katika nyumba chakavu ya familia hiyo, ni ya kutia simanzi, huku muda wote kelele za watoto hao zikisababisha utulivu upotee.

Mwandishi wetu Imelda Mtema, amefunga safari hadi Konde, Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba na kwenda kujionea hali halisi, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mwanamke huyo na mumewe, ambao wametoa simulizi ya kusisimua.

Leave a Comment