×

Mume, Mke Wakamatwa kwa Kuwauza Watoto Wao

VIKOSI vya usalama vya vya ulinzi wa raia nchini Nigeria vimemkamata mwanaume mmoja kwa jina, Elisha Effiong, kwa madai ya kupanga njama na mke wake ya kuwauza watoto wao wawili, Abasifreke Edet na Rachael Edet pesa za Nigeria – N700,000 (Tsh milioni 3.92) katika jimbo la kusini mwa nchi hiyo la Akwa Ibom.

 

Gazeti la Vanguard limechapisha taarifa ya Msemaji wa Kamishna wa Polisi, Umana Ukeme, jana Jumatano, akisema kuwa binti hao waliotaka kuuzwa na wazazi wao walikuwa na umri wa miaka sita na miaka minne.

 

Effiong ambaye anaishi nchini Cameroon na mke wake walikamatwa katika eneo la Uyo, Novemba 15, 2021, kufuatia taarifa iliyotolewa kwa siri huku wakijaribu kuwauza watoto wao Abasifreke na Rachael kwa sababu ya umasikini mkubwa alionao.

Leave a Comment