
Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania ( NACOPHA) leo limezindua Jukwaa la Taifa la Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania, ambao litawawezesha wanawake kupaza sauti zao kwenye sehemu husika na kuweza kusikika kwa haraka na sauti zao kufanyiwa kazi.

Jukwaa hilo limezinduliwa jijini Mbeya leo, ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi, yakiwa na kauli mbiu ya Kuzingatia Usawa,Kutokomeza Ukimwi,Kutokomeza magonjwa ya mlipuko.

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa mataifa kama,shirika la Unwomen,likiwakilishwa na Jacob Kayombo ambaye ni mratibu wa Programu ya UKIMWI UN women, akisisitiza kuwa itaungana bega kwa bega na NACOPHA, katika jukwaa hilo la wanawake walilolianzisha kwasababu limeweza kutoa nafasi ya wanawake wanaoishi na maambukizi kupaza sauti sehemu husika.

HABARI NA IMELDA MTEMA | GPL