×

Virgil Abloh Afariki Dunia

Mbunifu mahiri na maarufu wa mavazi kutoka nchini Marekani, Virgil Abloh (41) amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ndugu zake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram, imebainisha wazi sababu za kifo cha Virgil kuwa ni maradhi ya saratani aliyokuwa akikabiliana nayo kwa kupindi cha zaidi ya miaka miwili.

Virgil Abloh enzi za uhai wake alikuwa mkurugenzi wa Idara ya ubunifu wa Louis Vuitton Campany kwenye eneo la mavazi ya kiume.

Ambapo amehudumu kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga rasmi na kampuni hiyo mapema mwaka 2018.

Nje ya hapo Abloh alikuwa Mkurugenzi wa kampuni yake binafsi ya mavazi iitwayo Off-White aliyoifungua rasmi mnamo mwaka 2012.

Leave a Comment