×

Maua Sama Atisha Ile Mbaya

SEXY lady kunako Bongo Fleva, Maua Sama ametisha ile mbaya baada ya video yake ya Zai kutajwa kuwania tuzo kubwa duniani za New Vision International Awards ambazo hufanyika huko Uholanzi.

 

Maua; kupitia akaunti yake ya Instagram alitoa taarifa hizo kwa wafuasi wake na kuwweka wazi kwamba huwenda akahudhuria utoaji wa tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika huko Amsterdam nchini Uholanzi ifikao Desemba 20, 2021.

 

Amsterdam see you soon. Zai Nominated Best Music Video -New Vision International Awards. Asanteni kwa kuendelea ku-support muziki mzuri hii inakuja nyumbani asubuhi na mapema, nawapenda sana,” ameandika Maua.

 

Maua aliachia video ya Zai, Oktoba 20, mwaka huu na tangu kuachiwa kwake, imekuwa ni video pendwa kwa mashabiki wake.

Leave a Comment