
Tanzania imepokea shehena ya Chanjo aina ya Janssen Dozi 115,200 zitakazotumika kuchanja wananchi 115,200 kwa ufadhili wa Serikali ya Ubeligiji kupitia mpango wa COVAX Facility kwa lengo la kuwakinga wananchi dhidi ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya UVIKO-19.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa, Serikali itaendelea kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo ili kuwezesha wananchi kujikinga dhidi ya UVIKO-19.
Aidha Dkt Gwajima amewaagiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhamasisha jamii kujitokeza kupata chanjo na kujikinga kwa kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19.