×

Rais Samia: Nitaendelea Kuzunguka – Video

Rais Samia Suluhu Hassan amesema safari ya uwekezaji kuna njia ndefu na ndiyo maana wakati mwingine analazimika kutoka kwa ajili ya kutafuta wawekezaji katika nyanja mbalimbali ili waje kuwekeza nchini na kuliletea Taifa letu maendeleo.

Rais Samia amesema hayo leo Kigamboni Dar es salaam wakati was uzinduzi wa kiwanda cha vifaa vya umeme cha El Sewedy kinachomilikiwa na Wawekezaji kutoka Misri ikiwa ni chini ya wiki nne toka Rais Samia aende Misri kushawishi Wawekezaji waje kuwekeza Tanzania.

 

“Kama nimekubali kubeba mzigo wa kuongoza hii nchi kuna mambo kadhaa yaliyoelekezwa ndani ya Ilani niyatimize, sitayatimiza kwa kukaa ofisini Dodoma au Magogoni lazima nitoke niongee na watu niwashawishi waje kwetu na wakija nihakikishe mambo yamenyooka.

 

“Niliahidi kwamba tutajenga chuo kikubwa cha TEHAMA, nataka kuwaambia harakati za awali ziko tayari na muda wowote ujenzi wa chuo hicho utaanza ili vijana wetu wafundishwe mambo ya ICT na waweze kutumika vyema katika uwekezaji unaokuja.

 

“Safari ya wawekezaji kuja ni ndefu, bado nitaendelea kuzunguka na kuwaambia njooni Tanzania, nafanya hivyo kwa sababu ilani imenituma kama nimekubali kubeba mzigo wa kuongoza hii nchi kuna mambo kadhaa yaliyoelekezwa niyatimize,” Rais Samia Suluhu Hassan, Desemba 6, 2021 wakati wa kuzindua rasmi kiwanda cha Elsewedy, kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Leave a Comment