×

Vodacom Yazindua Kampeni ya ‘Show Love, Tule Shangwe” Msimu wa Sikukuu

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose (kulia ) akionyesha upendo kwenye uzinduzi wa kampeni mpya msimu huu wa sikukuu na Vodacom “Show Love, Tule Shangwe ” ambapo wateja wa Vodacom wataweza kujishindia zawadi mbalimbali mara wafanyapo miamala ya M-Pesa, ili kushiriki na kusambaza upendo wateja watapiga *149*01# au App ya M Pesa wataingiza namba za simu za ndugu na marafiki watakaopenda kugawana nao zawadi. Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom, Linda Riwa na Masta Shangwe.

 

 

 

3 DISEMBA 2021 – Dar es Salaam. Vodacom Tanzania Plc, kampuni ya teknolojia na mawasiliano inayoongoza nchini leo imezindua kampeni yake ya msimu wa sikukuu inayoitwa “Show Love, Tule Shangwe” inayolenga kuwezesha watumiaji wake kushinda zawadi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na televisheni, simu janja na pesa taslimu.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose (wapili kulia ) akionyesha upendo kwenye uzinduzi wa kampeni mpya msimu huu wa sikukuu na Vodacom “Show Love, Tule Shangwe ” ambapo wateja wa Vodacom wataweza kujishindia zawadi mbalimbali mara wafanyapo miamala ya M-Pesa, ili kushiriki na kusambaza upendo wateja watapiga *149*01# au App ya M Pesa wataingiza namba za simu za ndugu na marafiki watakaopenda kugawana nao zawadi. Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom, Linda Riwa, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni ( kulia ) na Masta Shangwe.

 

 

 

Ili kunogesha na ushirikiano katika kipindi hiki cha sikukuu, wateja watagawa na zawadi hizi na wapendwa wao.

Wafanyakazi wa Vodacom katika Pozi la shangwe baada ya uzinduzi huo.

 

 

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose alisema, “Nina furaha kubwa kuwatangazia uzinduzi wa kampeni hii ya Vodacom – ‘Show Love, Tule Shangwe’.

 

Kampeni hii inaendana na dhamira ya upendo na ushirkiano. Tuliwaahidi kuwa ‘Yajayo yanafurahisha’ na leo, kupitia uzinduzi huu tunathibitisha msemo wa Vodacom kuwa ‘Pamoja Tunaweza’ ambao unasisitiza jinsia mbavyo ushirikiano kati ya utu na ubinadamu na ubunifu unavyoweza kuzaa matunda makubwa.”

 

Kampeni hii ya wiki 6 itakuwa na uwepo wa mtu maalum aitwaye “Masta Shangwe” – atakaye jitokeza hapa na pale nchi nzima kuwazawadia wateja wa Vodacom zawadi nyingi za papohapo.

 

“Masta Shangwe atakuwepo kuwazawadia wateja wetu walioishi Maisha ya kidijitali, kutakuwa na zawadi za papo hapo kwa wateja pindi watumiapo huduma kama vile M-Pesana App ya ‘My Vodacom” kusambaza upendo kwa familia na marafiki kwanjia ya kutuma pesa au kuwanunulia bando za mawasiliano” alisema Sitholizwe.

 

Akielezea zaidi jinsi watumiaji watakavyonufaika na kampeni hii, Linda Riwa, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania alisema, “Wakati huu, watu wengi husherehekea kwa kukusanyika kifamilia, kununua na kupeana zawadi na kusafiri mikoani. Kwetu Vodacom, tunataka kuwezesha wateja wetu kusherehekea msimu huu kupitia bidhaa na huduma zetu.

 

Wateja watahitajika kutumia huduma zetu. Kama vile kumnunulia bando Rafiki au kugawa sehemu ya bando baada ya kujinunulia mwenyewe; Kufanya miamala kupitia M-Pesa kama kulipia huduma au kumtumia mtu pesa;

 

Kucheza mchezo wa “Tikisa Ushinde” au kujisajili huduma ya POA TV.“ Kampeni hii imepangwa kuendelea hadi mwezi wa kwanza mwakani na kutakuwa na zawadi za kila siku, wiki, mwezi na pia kutakuwa na zawadi kuu.

 

Zawadi hizo ni pamoja na:

  • Kurejeshewa Pesa kwenye akaunti ya M-Pesa baada ya kulipia huduma
  • Muda wa maongezi
  • Bidhaa za nyumbani
  • Simu za mkononi
  • Malipo ya LUKU
  • Vifurushi vya DSTV
  • Kulipiwa tiketi ya usafiri mikoani
  • Vocha za kununulia bidhaa madukani
  • Malipo ya ada za shule.

Ili kushiriki na kusambaza upendo, wateja watapiga *149*01# au watatumia App ya M-Pesa, wataingiza tamanio na namba za simu za ndugu au marafiki wanaotaka kugawana nao zawadi.

Leave a Comment