
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene anatarajiwa kuziteketeza kwa moto silaha zaidi ya 5,000 zilizokua zinamilikiwa kiholela.
Kwa mujibu wa Wizara ya mambo ya Ndani, tukio hilo litafanyika leo Ijumaa, Desemba 10, 2021 katika viwanja vya kulenga shabaha vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) vilivyopo Kunduchi, Dar es Salaam.
Aidha, tukio hili linakuja ikiwa ni baada ya Jeshi la Polisi kufanyika msako wa kuzikamata silaha hizo kutoka kwa majangili, watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya uhalifu na wananchi wa mikoa mbalimbali kutokana na kutengenezwa kiholela na kuzimiliki bila kuwa na vibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.