×

Polepole Ataka Serikali Iwajibu Wanaohoji Deni la Taifa Awamu ya Tano – Video

MBUNGE wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amewataka viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza na kuwajibu watu wanaohoji kuhusu pesa zilizokopwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wajibiwe.

 

Polepole amesema hayo leo Jumamosi, Desemba 11, 2021 wakati akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa LRHC, Kijitonyama, Dar es Salaam.

 

“Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya.

 

“Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli?

 

“Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya.

 

“Mtu anakuja anasema deni la Taifa limeongezeka hata hajafanya uchambuzi, hata kama ana umbo kubwa tumjibu. Imeibuka ishu ya Bandari ya Bagamoyo namshukuru Mzee Mangula alijitokeza akasema kwenye Ilani tuliahidi gati sio bandari, japo mawazo yanaweza kuboreshwa.

 

“Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea.

Leave a Comment