
Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Mwango Nzioka mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa akifanya kazi ya kuendesha bodaboda, amemuua mpenzi wake, Mercy Gichuhi kisha naye kujiua, tukio lililotokea katika eneo la Mitaboni, Kaunti ya Machakos nchini Kenya.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo liligundulika na mmoja kati ya wasichana waliokuwa wakifanya kazi ya kuuza baa na marehemu Mercy, ambao walifika nyumbani hapo kuchukua funguo baada ya kuona mwenzao hajafika kazini asubuhi kama kawaida, huku akiwa na funguo za ofisi.
Kwa mujibu wa baba wa marehemu ambaye anafanya kazi ya ulinzi, Peter Kaloki mara ya mwisho kumuona mwanaye na mchumba wake huyo ambaye alikuwa akiishi naye, ilikuwa ni Jumatatu usiku ambapo walirejea kutoka kwenye matembezi ya jioni huku kukiwa hakuna dalili zozote za ugomvi kati yao.