×

“Vibe la Christmas, Tecno Yatosha” Yazinduliwa Rasmi

Habari njema imeanikwa kwa Watanzania na zaidi sana kwa wale watumiaji simu janja, Kampuni TECNO imewaletea wateja wake na wananchi wote promosheni baab’kubwa iliyopewa jina la “VIBE LA CHRISTMAS, TECNO YATOSHA” ambayo imezinduliwa rasmi leo ambapo wateja watakaonunua simu za TECNO katika msimu huu wataondoka na zawadi za kutosha.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja mMauzo wa TECNO, Ms. Mariam Mohammed amesema “Msimu huu wa sikukuu chochote unachotaka kuwapa zawadi ndugu, jamaa na marafiki zako msimu huu wa sikukuu, utakipata TECNO, unachotakiwa kufanya nunua simu yoyote ya smartphone kutoka TECNO basi na sisi hatutawezi kukuacha hivi hivi”.

“Mwisho wa mwezi huu ndio kutakuwa na droo ya kushinda zawadi kubwa ya friji, mashine ya kufulia, microwave na zawadi zengine mbalimbali. Zawadi hizi za droo kubwa zinawalenga wale wateja wote watakao nunua simu za CAMON 18 Series na SPARK 8 Series.

Promo hii itakuwa nchi nzima katika maduka ya TECNO yenye promosheni ambapo zawadi zitatolewa papo hapo dukani kwa wateja watakao nunua simu za POP Series, SPARK Series na CAMON Series. Hii ni desturi ya kampuni ya TECNO kuwa na promosheni kubwa kipindi iki cha mwisho wa mwaka ambapo ni mda mahususi kabisa wa kutoa shukrani kwa njia ya zawadi kwa marafiki, ndugu, jamaa na wana wamilia yako kiujumla,” alisema Ms. Mariam.

Kufahamu zaidi juu ya promotion hii au kufahamu duka gani la kutembelea sahihi lenye promosheni wapigie kwenye namba zao 0744545254 au 0678035208.

Leave a Comment