×

Mayele Afungukia Ishu Yake na Hennock Inonga

SHAMBULIAJI Mpya wa Yanga Mkongomani Fistoni Mayele, amesema kuwa yeye na Beki Mkongomani
wa Simba Hennock Inonga ni washkaji wakubwa sana.

 

Wawili hawa wameiteka mitandao ya kijamii kwenye Dabi ya Kariakoo kutokana na jinsi ambavyo
walipambana kwenye mchezo huo.


Inonga alionekana kumpania zaidi Mayele asiifunge timu yake, huku akisindikiza nje wakati anatoka uwanjani na
nafasi yake kuchukuliwa na Makambo.


Akizungumza na Championi Jumatatu Mayele amesema kuwa Inonga ni mshikaji wake mkubwa wana wanajuana
muda mrefu “Inonga ni rafiki yangu sana na hatujawahi kucheza timu moja ila huwa tunakutana kwenye
 majukumu ya timu ya Taifa.


“Mimi na yeye tunajuana sana na ni mshikaji wangu, hii ilikuwa kazi na ni lazima kila mmoja
aonyeshe kiwango chake,” alisema mshambuliaji huyo.

STORI: CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave a Comment