
BEKI kisiki wa Wananchi, Kibwana Shomari na straika namba moja wa timu hiyo, Fiston Mayele ni miongoni mwa nyota wanne wa Klabu ya Yanga ambao wanakabiliwa na majeruhi ndani ya kikosi hicho. Mwingine ni Yusuf Athumani pamoja na Yacouba Songne ambae alifanyiwa upasuaji wiki chache zilizopita nje ya nchi.
Katika taarifa yake Klabu ya Yanga haikuweka wazi ni majeruhi gani hasa yaliyowakumba nyota hao hasa katika nyakati hizi muhimu wakiliwinda taji la Ligi Kuu Bara. Vile vile haijulikani watakaa nje kwa muda gani lakini taratibu za kutibiwa nje ya nchi zinaendelea.
Soma kwa kina taarifa iliyotolewa na Yanga;
