×

China Yapangua Tuhuma za Kutengeneza Silaha Kudhibiti Ubongo

China imelaani uamuzi wa Marekani wa kuorodhesha kampuni na taasisi zake 34 kuwa zinatengeneza silaha za “kudhibiti ubongo” ikitaja madai hayo kwamba “hayana msingi kabisa.”

Mashirika 34, yakijumuisha Chuo cha Sayansi ya Kijeshi cha China (AMMS), yaliongezwa kwenye orodha isiyoruhusiwa Jumatano – na kuwazuia kununua teknolojia yoyote ya Marekani.

Kabla ya nyongeza za Jumatano, orodha hiyo tayari ilikuwa na kampuni zaidi ya 260 za Wachina, pamoja na mtengenezaji maarufu wa simu – Huawei.
Ubalozi wa China huko Washington, DC ulipuuza uamuzi wa Marekani kama “ukandamizaji usio na msingi” na kuapa kuchukua “hatua zote muhimu” kulinda biashara za China.

Leave a Comment