×

Ataka Kutapeli Familia ya Mtoto Aliyefufuka, Yamkuta

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema wanamshikilia Charles Christopher kwa kutaka kuitapeli familia ya Mtoto anaedaiwa kufufuka Leonard Morisha Mkazi wa katika Kijiji cha Ngemo Wilaya ya Mbogwe kiasi cha shilingi milioni tatu za Kitanzania.

 

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya kufikishwa kituo cha polisi walimuweka chini ya ulinzi huku wakiendelea kufanya uchunguzi wa kubaini lengo lake.

 

“Huyu Charles alienda katika Kijiji cha Mgeni kule ambako tulitoa taarifa ya mtoto aliyekuwa amefariki Mwaka 2017 kisha akaonekana mwaka huu.

 

“Alipofika kwenye familia hiyo akajitambulisha kama yeye ni Ofisa Upelelezi ameagizwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe na kwamba wamejadiliana na DC kuwa wamefanya kazi kubwa sana kuanzia kupeleka mtoto hospitali na kufukua kaburi hivyo wapewe hela,” amesema Mwaibambe.

 

Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji hicho Bahati Laurent amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika kijiji chake huku akisema Serikali ya Kijiji ilitoa uamuzi wa kumpatia adhabu ya kumchapa viboko kijana huyo tapeli.

Leave a Comment