×

Kamanda ‘Nyakuanyakua’ Aja na Hii Mpya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu maarufu Kama kamanda Nyakuanyakua amekuja na kauli mpya aliyeipa jina la “SAFISHA SAFISHA UHALIFU MOROGORO WASHA MOTO” yenye lengo la kupambana na uhalifu mkoani humo.

Akizungumza wakati wa operesheni maalumu aliyoifanya katika barabara ya Morogoro-Dodoma usiku wa kuamkia leo Desemba 23, ili kuzungumza na madereva wa magari makubwa ya mizigo na abiria kamanda Musilimu amesema mkoa wa Morogoro ni kisiwa cha amani hivyo uharifu wa aina yeyote hautakubalika.

“Madereva wanalalamika Morogoro tunafanya operesheni nyingi, Ni kweli na tutafanya hivyo hadi pale madereva watakapo kubali kufuata sheria za Usalama barabara mfano juzi imetoka ajali eneo la mkambarani lakini chanzo Cha ajali ni uzembe wa dereva alizidiwa na usingizi hivyo hatutakubali uzembe wao ugharimu maisha ya watanzania,” amesema Kamanda Musilimu.

Leave a Comment