×

Aliemuua Mama Yake Marekani Akamatwa Bongo

 

MWANADADA WYLUVA Ngongoseke, Mtanzania ambaye mama yake mzazi Catherine Ngongoseke (60) amekutwa akiwa ameuwawa kwa kuchomwa visu nyumbani kwake Texas nchini Marekani, ndiye anayetajwa kama mtuhumiwa namba moja katika mauaji hayo.

 

Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia RPC wa Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema mwanadada huyo anahisiwa kufanya mauaji hayo na kukimbilia Dar es Salaam, Tanzania na kujificha.

 

Mpaka sasa vyombo vya usalama vya nchini Marekani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini Tanzania wamefanikiwa kumkamata Wyluva katika maeneo ya Mbezi Beach, Dar akiwa amejificha kwa mjomba wake Peter Ngongoseke na sasa wapo kwenye mpango wa kumrudisha nchini Marekani ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Leave a Comment