
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ugumu uliopo kwa timu hiyo kusepa na taji la Ligi Kuu Bara ni ushindani ambao wanakutana nao kwenye mechi wanazocheza.
Yanga inapambana kutwaa taji la ligi ambalo lipo mikononi mwa Simba, ilikuwa na pointi 23 ikiwa nafasi ya kwanza kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Biashara United uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa kila timu inahitaji ushindi hivyo haitakuwa rahisi kwa timu hiyo kutwaa ubingwa.
“Malengo ya kutwaa ubingwa yapo lakini haitakuwa rahisi kuweza kuyatimiza hasa ukizingatia kwamba timu zote zipo imara na zinahitaji ushindi na zinapokutana na Yanga zimekuwa zikicheza kwa nguvu kubwa,” alisema Nabi.
LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam