×

Maajabu: Ukweli Wa Mti Uliogoma Kukatika – Video

Mti wa ajabu wa asili uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ambao umeshindwa kukatika na kubaki katikati ya barabra umekuwa kivutio kwa watalii kwa kutaka kuuona na kuushika kutokana na historia yake kutumiwa kufanya matambiko mbalimbali na jamii ili kutatua ama kusaidia hitaji husika.

 

Mti huo aina ya Marula umekuwa kivutio kwa watu mbalimbali wanaofika kutembelea hifadhi hiyo, na kulazimika eneo hilo kuwekwa barabara mbili pacha na walipojaribu kuukata kushindikana kuondolewa wakati upanuzi wa barabara ndani ya hifadhi hiyo ya Nyerere ikitokea Kijiji cha Mloka wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

 

Afisa Uhifadhi Mwandamizi, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (TANAPA) Seth Mihayo, akizungumzia mti huo amesema umekuwa kivutio kwa sababu wakati wa upanuzi huo wa barabara licha ya kutumia vifaa vya kisasa kama magreda ya kukata miti mikubwa mti huo ulishindikana kukatika na badala yake vifaa hivyo licha ya kuwa vya kisasa lakini viliishia kuharibika na mti kuendelea kubaki.

Leave a Comment