×

P-Square Wawapigia Magoti Mashabiki

Wasanii mapacha kutoka pande za Nigeria, Peter na Paul Okeye almaarufu P-Square wamepiga magoti mbele ya mashabiki wao na kuomba msamaha kwa mashabiki wote duniani wakati wakiendelea na show yao iliyofanyika nchini humo katika ukumbu wa Eko Convention Centre kupitia Music Tour yao waliyoipa jina la ‘’P Square Reactivated’’.

 

Ikumbukwe, wawili hao walitengana tangu mwaka 2017, kutokana na tofauti zao ndani ya familia.

 

Baadaye mwaka 2021, P-Square waliondoa tofauti zao na kuungana tena katika hafla ya kusherekea ‘birthday’ yao kwa kutimiza miaka 40.

 

Wimbo gani wa P-Square unaukubali sana?

Cc; @bakarimahundu

 

Leave a Comment